DC Korogwe Aagiza Jeshi la Polisi Kuwasaka Waliotega Jiwe Kwenye njia ya Treni


Mkuu wa Wilaya ya Korogwe  ameiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo kuchunguza Watu waliohusika na dalili za kutaka kuhujumu miundombinu ya reli.

Gwakisa ametoa kauli hiyo baada ya Watu wasiojulikana kutega jiwe kwenye njia ya reli hali ambayo ingeweza kuleta athari kwa treni ya abiria inayopita kwenye eneo hilo.

“Tukio kujitokeza mara mbili haivumiliki, naagiza Polisi chunguzeni kujua waliohusika na ile hujuma, Watu wametega jiwe kwenye njia ya treni, tambueni treni imebeba Watanzania wenzetu, undeni vikundi vya vijana viwe vinakagua kila treni inapotaka kupita”-DC Korogwe
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad