Dhamana kwa Kesi ya Uhujumu Uchumi Yajadiriwa Bungeni


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amesema kwa kuwa kesi za uhujumu uchumi hazina dhamana ipo haja sasa kwa wabunge na Bunge kutunga sheria ya marekebisho na kubadilisha pale ambapo itaona panafaa.

Hayo ameyabainisha leo Januari 30, 2020, Jijini Dodoma, kwenye Mkutano wa 18, Bunge la 11, Kikao cha Tatu, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Sabrina Sungura, lililohoji sababu ya vijana wengi wakiwemo kina Tito magoti kukutwa na kesi za uhujumu uchumi, na kukaa mahabusu muda mrefu, je Bunge halioni kama ni muda mwafaka sasa kufanya mabadiliko ya sheria ya uhujumu uchumi ili kuwapa nafasi Majaji na Mahakimu ambao wamekuwa wakiendesha kesi hizi ili waweze kutoa dhamana.

"Kuhusu suala la mabadiliko ya sheria ya uhujumu uchumi, nadhani ni Mamlaka ya Bunge hili kutunga sheria na kubadilisha pale ambapo inaona panafaa, na kama kuna utaratibu mwingine wa kuleta hoja binafsi ili sheria hii ya uhujumu uchumi, iweze kubadilishwa" amejibu Mhandisi Masauni.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad