Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetoa miezi miwili kwa pande mbili za familia za Marehemu Erasto Msuya zenye mgogoro wa kugombea mali zilizoachwa na Bilionea huyo kuondoa tofauti. Mahakama hiyo imezielekeza pande hizo kupeleka mrejesho Mahakamani baada ya muda huo kupita
Jaji wa Mahakama hiyo, Johannes Masara, alisema mahakama imeridhia ombi la Ndeshukulwa Msuya, la kuomba mahakama kuondoa shauri lake la mirathi kwa muda ili familia hizo zifanye mazungumzo
Ndeshukurwa alisema uamuzi wa mahakama umetenda haki, na umezingatia maslahi mapana ya pande zote mbili na anaamini jambo hilo, litamalizika na watoto wa Bilionea Msuya watapata haki yao ya msingi
Ndeshukurwa, mama mzazi wa Bilionea Msuya anapinga Miriamu Mrita, mke wa Msuya kuwa Msimamizi wa Mirathi, akidai kuwa ameshindwa kugawanya mali kwa kipindi cha miaka saba tangu kifo cha Msuya
Miriamu yuko Mahabusu tangu Agosti 2016 akikabiliwa na kesi ya mauaji ya wifi yake, Anet Msuya
Bilionea Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 mwaka 2013 Wilayani Hai, Mkoani Kilimanjaro