Fatma Karume na Mdee wamtolea povu Mtatiro kwa kuzuia wazazi kufanya sherehe



Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume na Mbunge wa jimbo la Kawe (Chadema), Halima Mdee wamemtolea povu Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro kwa kitendo cha kuwazuia wazazi wasiwafanyie watoto wao sherehe nyumbani baada ya kuhitimu darasa la saba.

Fatma alisema Mtatiro anapiga marufuku watu kusherehekea mafanikio ya watoto wao je ni sheria gani ambayo inampa hayo mamlaka.

“Acheni kuwafanya jamaa zenu watumwa. Waheshimu japo kidogo kwa utu wao mnakera sana,” alindika Fatma katika ukurasa wake wa Twitter.


Fatma Karume
Fatma aliandika ujumbe huo baada ya taarifa ya Mtatiro kupiga marufuku sherehe za wanafunzi wanaohitimu darasa la saba zinazofanywa na wazazi nyumbani na kudai kuwa sherehe itakuwa ni moja katika shule husiku.

Baada ya taarifa hiyo Fatma alimuandikia ujumbe huu “Marafiki huniambia ‘unapigania utawala wa sheria. Hawatoelewa maana yake milele’ @Julius _Mtatiro unapiga marufuku watu kusherehekea mafanikio ya watoto wao? sheria gani inakupa mamlaka hiyo? acheni kuwafanya jamaa zenu watumwa. waheshimu japo kidogo kwa utu wao. Mnakera sana,”

Halima James Mdee
Naanza KUAMINI, ukisha UNGA JUHUDI... AKILI zinabaki ULIKOTOKA! Huu ni UJINGA wa Kiwango cha LAMI!! 🚮🚮 

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mila za huko ni zingine mama fatuma we nenda kaishi nao mwaka ili uzijue. Nikiwa kasichana nilikuwa nakutana kisimani na vitito vingine vidigo kuliko mimi vikija kuchota maji. Mimi niliambiwa yule nikaonyeshwa (kwa kidole) kaolewa. Maskini kalikua pengine hata miaka kumi bado. Kalikua kanyonge, hakana ujasiri wa kujumuika na watoto wengine, ni kama aliyenyanyapaliwa. Sasa mama karume mila hizi huenda ndo mziizi ya alichokiona dc mtatiro. Mtoto yule na wengine walihitaji mkombozi

    ReplyDelete
  2. Mtu nilikuwa chini ya miaka 7 mtu alimwambia baba yangu mimi nataka kulomba huyu naye baba hakumkawiza akamuuliza wanalomba mtoto kama huyu?!

    ReplyDelete
  3. Alitahayari mwenyewe

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad