Hamisi Kigwangalla “Walipanga Kuniua Sasa Naingia Vitani”


Leo January 21,2019 Waziri Kigwangalla ameandika katika ukurasa wake wa twitter  “Kuna limit kwenye uvumilivu, uvumilivu ni hekima lakini uvumilivu wako usionekane kuwa ni ugoigoi ama upuuzi, kuna Watu wamenijaribu kwa muda mrefu sana, sasa wamefanikiwa kunifikisha ukomo wa uvumilivu wangu, naogopa uongo usijegeuka ukweli”.

“Nafahamu Watu wema,Watendahaki, Wanamageuzi wamewahi kuumizwa kwasababu ya uvumilivu wao,kuna wakati nilikata tamaa nikataka kujiuzuru uongozi ila nikafikiria upya, kama Watu wema wanaopigwa fitna na majungu wakisusa na kuacha kazi za kujenga Nchi,nani atakayefanya?”- Kigwangalla

“Ukiwa Waziri wa Maliasili na Utalii ukakuza idadi ya Watalii kwa kasi, ukaongeza mchango wa sekta yako kwenye pato la Taifa,ukadhibiti ujangili, ukaufanya utalii kuwa ‘fashionable’, badala ya kupendwa unashambuliwa, ukijiziulu ni kuwapa ruhusa kuendelea na mambo yao”-Kigwangalla

“Waliwahi kupanga mbinu za kunidhuru, pengine kuniua Mungu akanisalimisha, walishindwa kuniua, hawatoniangusha leo, naingia vitani kwa silaha zote, usiombe kunifikisha hapa, Mimi hupigana vita bila kujali nani atadhurika, alietaka vita ameipata” Kigwangalla
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad