Kila jambo lina pande mbili, upande wa uzuri na upande wa ubaya, lakini katika kufanya maamuzi basi ni vyema kuegemea upande wenye mazuri zaidi kuliko mabaya.
Katika uchunguzi mdogo niliofanya usio rasmi katika suala la mahusiano hususani katika kipengele cha kuchepuka kuna baadhi ya mambo yamebainika, hebu tujifunze kwa lengo la kujenga zaidi.
Kuchepuka ni aina nyingine ya usaliti anaoufanya mtu kwa mpenzi wake, japo wahenga walinena acha michepuko baki njia kuu, michupeku hutokea katika nyanja zote za mahusiano, kuanzia kwenye uchumba hadi kwenye ndoa, sababu huwa ni nyingi ambazo hupelekea mwanaume au mwanamke kufanya usaliti, japo kiwango hitofautiana..
Sasa katika kuchepuka huwa kuna mambo mengi yanayoibuka, tuangalie faida na hasara za kuchepuka, ni katika kujifunza ili kuchagua njia iliyobora, na kuacha kujisahau.
HASARA1. Kuambukizwa Magonjwa ya zinaa kama kinga haitatumika.
2. Kusahau au kuacha kabisa kuhudumia familia na kumuhudumia mchepuko, wapo waume za watu wanaishi nyumba za kupanga na familia zao la wamewajengea nyumba michepuko yao, au wengine wamewanunulia magari michepuko yao huku mke wke akiwa anahangaika na madaladala.
3. Kuishi kwa hofu na mpenzi wako kwani nafsi inakusuta na hofu ya siri yako ya mchepuko kuvuja.
4. Gharama zitapanda kugaramikia Familia na mchepuko.
5. Kukosa muda na familia yako
6. Kutokua huru na mpenzi wako kwani kuna kitu anaficha, na utakua hauko huru na Simu yako.
7. Kua mkali/kuboreka na familia kwani atahisi wanakubana usijiachie na mchepuko.
8. Kutokua huru kutoka na Familia hususani kama Mchepuko utakua jirani.
9. Kukwepa ibaada kwani Dhamila inakuhukumu.
10. Kutofurahi unyumba na Mpenzi wako hasa akiwa anazidiwa ufundi na Mchepuko na ndio hivyo Mara nyingi.
FAIDA1. Inapunguza msongo wa mawazo hasa kama wpenzi wako hakujali.
2. Inadumisha mahususiano kwani inapunguza wivu wa kijinga hasa kama wote mnachepuka.
3. Inaleta uvumilivu kwenye mapenzi huwezi kumuhukumu mpenzi wako harakaharaka kwani na wewe hauko Sawa
4. Kupata vionjo mbalimbali kwani michepuko huwa inajituma sana.
5. Inaongeza Mori wa kazi hasa kama mchepuko wako upo Hapo kazini.