Hii Hapa Historia ya Marehemu Kobe Bryant...



Mwaka 1996, Kobe Bryant aliingia uwanjani kwa mara ya kwanza akiwa na miaka 18, hakuwa na umaarufu, mwaka 2016 alistaafu akiwa ni moja ya majina makubwa zaidi kuwahi kutokea kwenye ulimwengu wa kikapu.

Baada ya miaka 20 ya kuchezea timu ya LA Lakers na kushinda ubingwa wa ligi mara tano, namba za jezi mbilia mbazo alizitumia kwa vipindi viwili tofauti , 24 na nane zilistaafishwa kwa heshima yake. Hakuna mchezaji mwengine yeyote ambaye atapewa kuzivaa.

Kifo chake katika umri wa miaka 41 kimeshtua wengi. Binti yake mkubwa Gianna, 13, ni miongoni mwa watu wanane ambao wamefariki pamoja na nyota huyo baada ya helikopta binafsi ya mchezaji huyo kuanguka jana Jumapili.

Bryant aliyezaliwa Agosti 23, 1978 ameacha mke na watoto wakike watatu, mdogo kabisa akiwa amezaliwa mwezi Juni mwaka jana.

Kutokana na ubora wake uwanjani alipewa jina na Black Mamba, nyoka mkali apatikanaye katika maeneo mengi barani Afrika.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) Adam Silver, Bryant si tu ni miongoni mwa wachezaji bora tu kuwahi kutokea bali alishawishi wachezaji wengi zaidi kuingia kwenye mchezo huo ulimwenguni kote.

"Familia ya NBA imefadhaika sana na msiba huu mzito wa Kobe Bryant na binti yake Gianna," amesema Silver.

"Kwa misimu 20, ametuonesha unachoweza kufanikisha pale ambapo kipaji cha hali ya juu kinapochanganyika na ari kubwa ya ushindi. Alikuwa ni moja ya mchezaji wa kiwango cha juu kuwahi kutokea.

"Kubwa zaidi, atakumbukwa kama mchezaji mwenye ushawishi mkubwa ambaye aliwafanya watu kunyanyua mpira wa kikapu na kushindana kwa kadri ya uwezo wao.

"Alikuwa mwema na mwenye busara na alitumia uzoefu wake wote katika kusambaza maarifa kwa vizazi vya wachezaji wa baadae, na akawa mwenye furaha zaidi kwa kuhamisha mapenzi ya mchezo huo kwa binti yake Gianna."

Wakati wa hafla ya kumuaga baada ya kustaafu kikapu, mmiliki wa LA Lakers Jeanie Buss alimwambia: "Tulikutaka ujitume (kwa ajili ya klabu) lakini wewe uliutoa moyo wako wote jambo ambalo lilikuwa kubwa zaidi. Umeacha alama itakayodumu milele katika klabu hii."

Mafanikio ya Kobe katika nambari
48,637

Katika misimu ishirini aliyocheza ligi ya NBA, nyota huyo ameweka rekodi ya kucheza dakika 48,637 na kuwa mchezaji wa nane aliyecheza dakika nyingi zaidi.

Bryant, ambaye alicheza kwa mara ya kwanza msimu wa 1996-97 amefunga jumla ya alama 33,643 na kumfanya kuwa mchezaji namba nne mwenye alama nyingi zaidi nyuma ya Abdul-Jabbar (38,387), Karl Malone (36,928) na LeBron James (33,655), ambaye alimpiku Bryant nafasi hiyo siku ya Jumapili pia akiichezea Lakers.

Mwaka 2006 Lakers iliichapa Toronto Raptors vikapu 122 kwa 104. Bryant peke yake alifunga vikapu 81kwenye mechi hiyo. Mchezaji mwenye rekodi kubwa kuliko Bryant kwa mechi moja ni Wilt Chamberlain ambaye alifunga alama 100 mwaka 1962.

Idadi ya alama amabazo aliifunga Utah Jazz katika mechi yake ya mwisho kabisa ya NBA. Hiyo ilikuwa ni mara yake ya saba kufunga alama 60 au zaidi toka alipofanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka 2009.

Idadi ya michezo ambayo amefunga alama 50 na zaidi peke yake - ni wachezaji wawili tu wastaafu ndio wenye rekodi kubwa zaidi yake ambao ni Wilt Chamberlain ( mechi 118) na Michael Jordan ( mechi 31).

Bryant amecheza misimu yake yote 20 na klabu ya Lakers. Ni Dirk Nowitzki pekee ambaye kacheza misimu yake 21 na klabu ya Dallas Mavericks, ambaye ana rekodi ya kucheza misimu mingi zaid kwenye klabu moja ya NBA.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad