Hii ndio idadi ya vifaa vya NIDA vilivyoibiwa Arumeru, Jeshi la Polisi limeanza upelelezi


Jeshi la Polisi mkoani Arusha linaendelea na upelelezi ili kuwabaini watu waliohusika na wizi wa vifaa vya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), katika ofisi za NIDA zilizopo maeneo ya Arusha DC, wilayani Arumeru.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mratibu wa Polisi, wilayani Arumeru, Kamanda Mapunda, kupitia kwa Afisa Habari wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha, Abel Stanford, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, lililotokea usiku wa kuamkia leo Januari 6, 2020.

“Ni kweli kwamba kuna uvunjifu umefanyika maeneo ya Ofisi za NIDA hapo Arusha DC, wameiba Camera 2, Desktop 1, Laptop 2, ila Mratibu wa Polisi Arumeru yuko eneo la tukio anafuatilia, baadaye tutatoa taarifa kamili” amesema Abel.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad