Hii Ndio List Ya Vyakula Vinavyoongeza Hamu Na Nguvu Ya Kufanya Tendo la Ndoa
0
January 21, 2020
Hakuna binadamu asiyefahamu nini maana ya mapenzi na kama wapo basi ni wachache sana na wanaweza kuwa hawafahamu kwa maneno lakini kivitendo wanakuwa wanafahamu aidha kwa kuona, kusikia na hata kwa wao wenyewe kushiriki kwenye mapenzi hayo.
PILIPILI
Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho kutoka au kamasi kutoka. Kwenye pilipili kuna kitu kinaitwa capsaicin ambacho hufanya pilipili iwe na hali ya ukali ambao huwezesha ubongo kutoa homoni ya endorphins ambayo katika hali ya juu huleta mguso wa hisia za raha. Pia pilipili husisimua mfumo wa ufahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo huwezesha kumshwa haraka kimapenzi (kunyegeka) na pia ili ukiguswa au kubusiwa au kunyonywa au kupapaswa uweze kupata hisia kila sehemu
NAFAKA
Nafaka zina nyuzinyuzi (fibre) na sukari ngumu (complex sugar) ambazo kusaidia kutunza uzito wa mwili. Nafaka husaidia katika kuzalisha homoni za testosterone kwenye damu. Na pia nafaka huwezesha mtu kuwa na nguvu hatimaye kwenda masafa marefu wakati wa tendo. Kula nafaka nzima kama vile brown bread badala ya white bread, pia kula nafaka halisi badala ya cornflakes ni jambo zuri linalokuhakikisha afya njema na mahusiano mazuri ya ndoa yako
MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI.
Mlo wenye matunda na mboga za majani una matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi. Kwanza matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta na unene (cholesterol), kuongezeka kwa mafuta mwilini huzuia mzunguko wa damu kwa kubana mishipa ya damu. Pia kula matunda na mboga za majani huhakikisha balance ya uzito kwani unene (obesity) kwa wanaume kuna matokeo mabaya katika kuzalisha homeni za testoeterone na hatimaye jogoo kushindwa kuwika na kuwa na libido kidogo. Na pia wanandoa wanapozidi kunenepeana ndipo na hali ya kufurahia au kutaka au hamu ya tendo la ndoa huzidi kupungua.
TANGAWIZI
Tangawizi ni chakula ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume. Inaweza kuliwa mbichi, au kupikwa au kuanikwa na kuwa kama unga.
ASALI
Asali ina madini yanayoitwa boron, ambayo husaidia mwili kutumia homoni ya estrogen ambayo ni homoni inayohusika na viungo ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke. Pia kuna utafiti unaoonesha kwamba asali huongeza nguvu, kitendo ambacho kitapelekea mwanamke kuwa uwezo na hamu ya tendo la ndoa au libido.
KARANGA
Karanga huhusika moja kwa moja na kutunza mfumo wa mzunguko wa damu kuwa na afya (vascular system). Pia mfumo wenye afya (mzunguko wa damu) katika uke na uume huwezesha mwanaume na mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa zuri. Pia karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika usalishaji wa mbegu za mwanaume.
OYSTERS
Huwa na kiasi kikubwa sana cha madini ya zinc na haya madini ndiyo huhusika zaidi na uzalishaji wa homoni ya testosterone kwa wanaume. Pia imethibitika kwamba wanaume wenye ukosefu wa madini ya zinc huwa na matatizo ya nguvu za kiume na wakati huohuo kuwa na madini mengi ya zinc mwilini huongeza kiwango cha shahawa.
SOYA
Pamoja na kuwa na kiwango kidogo sana cha fat na pia kuwa na kiwango kizuri cha protein, soya zina phytoestrogens ambayo husaidia sana wanawake ambao wamefikia menopause kutengeneza homoni estrogen ya ziada. Husaidia uke kuwa laini (wet, lubricated) mwanamke akisisimliwa wakati wa tendo la ndoa.
CHOCOLATE
Chocolate ina phenylethylamine, kemikali ambayo husababisha hisia za furaha wakati wa mwanamke au mwanaume kufika kileleni
Tags