KUFUATIA madai kuwa, baadhi ya wasichana wanaofanya biashara ya kuuza mihogo, karanga na nazi kwenye foleni za magari na mitaani jijini Dar, wanajihusisha na biashara ya kujiuza, Kikosi cha Operesheni Fichua Maovu (OFM) kiliingia kazini na hiki ndicho kilichobainika.
MADAI YA AWALI
Baadhi ya mashuhuda walioongea na Risasi Jumamosi awali walidai kuwa, akina dada hao wawapo kwenye biashara hiyo, ukiwataka pia kwa huduma ya ngono wamekuwa ni wepesi kukubali kutokana na hali ngumu kimaisha. “Hawa akina dada unaowaona wanauza mihogo kwenye mabeseni wanapiga madili pia ya kujiuza, ukiwa kwenye gari au mtaani kisha ukamtaka unaweza kuondoka naye au anakupa namba yake kisha baadaye unamtafuta, mnamalizana,” alidai kijana mmoja anayefanya kazi ya umachinga kwenye mataa ya Ubungo jijini Dar.
Kamanada wa OFM na muuza mihogo.
OFM KAZINI
Kufuatia madai hayo kushika kasi, Kamanda wa OFM akiwa ndani ya gari lake maeneo ya Stendi ya Mawasiliano kuelekea Ubungo, alikutana na dada mmoja aliyejaaliwa shepu bomba akiwa anauza mihogo na mazungumzo yakawa hivi:
OFM: Shilingi ngapi mhogo?
Mdada: Kipande au mzima?
OFM: Kipande tu. Mdada: Kuna kipande cha 200, 500 na 1,000. Karanga na nazi pia zipo, si unajua tena! OFM: Nipe kipande cha mia tano na karanga lakini pia nakutaka na wewe, unasemaje?
Mdada: Aka! Sasa hivi niko kazini.
OFM: Basi nipe namba yako, nitakutafuta baadaye. Mdada huyo muuza mihogo huku akijichekesha akataja namba yake, OFM akaisevu.
MUUZA MIHOGO WA PILI
Siku nyingine kamanda wa OFM akiwa kwenye mizunguko yake maeneo ya Sinza-Mapambano jijini Dar alikutana na mdada mwingine muuza mihogo na mazungumzo yakawa hivi:
OFM: (Huku akionekana kum changamkia kana kwamba wanajuana) nataka kipande kidogo cha nazi na muhogo pamoja na wewe mwenyewe, unasemaje?
Mdada: Mh! Wewe ule kwanza mihogo na karanga zako kisha unitafute baadaye.
OFM: Baadaye tutaonana vipi sasa?
Mdada: Simu yangu imezima chaji, niachie namba yako basi halafu nitakutafuta. OFM akamuachia namba kisha wakaagana. Saa 2.30 usiku Katika kutaka kuthibitisha kama kweli akinadada hao wanafanya biashara hiyo ya kujiuza, ilipofika saa 2.30 usiku, kamanda wa OFM alimpigia simu yule dada wa kwanza, mazungumzo yakawa hivi;
OFM: Mambo?
Mdada: Poa, nani?
OFM: Najua huna namba yangu, mimi tulikutana pale Ubungo mataa, ukanipa namba yako.
Mdada: Aaa! Nimekukumbuka, niambie, nakusikiliza.
OFM: Ni hivi, mimi nimevutiwa na wewe, nakutaka kimapenzi, nikuandalie shilingi ngapi?
Mdada: Mh! kwani uko wapi?
OFM: Hapa Mwenge. Vipi unaweza kuja?
Mdada: Saa hizi itakuwa ngumu maana naishi mbali, tufanye kesho. Mwingine aingia mzimamzima Katika utafiti huo, OFM ilifanikiwa kukutana na dada mmoja anayeuza mihogo maeneo ya Buguruni Chama na alipotakiwa kutoa huduma ya ngono aliweka wazi kuwa, kama ni kulala aandaliwe 20,000 lakini kwa ‘short time’ ni 5,000!
Chanzo: Global Publishers
Kwani kuna shida gani kama mtu akijiuza? Si anauza mwili Wake sio wa mtu
ReplyDeleteBora anaeuza mwili wake kuliko jambazi anaua bula hatia
ReplyDeletetatizo tunasahau gharama za kuwahudumia wanapopata maambukizi ya vvu, pia tunapoteza nguvu kazi
ReplyDeleteDaaa
ReplyDeleteUlimshawishi. Yeye alikuwa anauza mihogo. Ulitake advantage kupitia ufukara wake. Tubadili Gia. Mzee makonda saidia kina dada hao dhidi ya walaghai hao. Wawekee mitego kama Ile ya takukuru. Na kwa kila atakayenaswa na mitego dada mhusika apewe zawadi. Hivi ndivyo tutakavyotokomeza vitendo vya uasherati na laana ndani ya nchi yetu.
ReplyDelete