Iran: Wachunguzi wa ajali ya ndege wamesema rubani hakutoa ishara ya hatari



Rubani wa ndege ya Ukraine iliyoanguka nchini Iran hakutoa taarifa ya kuomba msaada na alikuwa akijaribu kurejea katika uwanja wa ndege ndipo ndege hiyo ilipoanguka, kwa mujibu wa ripoti ya awali ya Iran iliyotolewa leo katika mkasa uliosababisha watu 176 kufariki dunia.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa hali ya dharura ilitokea kwenye ndege hiyo chapa Boeing 737 inayoendeshwa na shirika la ndege la Ukraine mapema siku ya Jumatano asubuhi, wakati ilipoanguka muda mfupi tu baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Imam Khomeini mjini Tehran.

Wakati huo huo Rais Volodymyr Zelenskiy wa Ukraine amesema wachunguzi wa ajali hiyo kutoka nchini mwake wamewasili nchini Iran kusaidia katika uchunguzi huo.

Pia rais Zelenskiy amesema anapanga kumpigia simu Rais Hassan Rouhani wa Iran juu ya ajali hiyo pamoja na uchunguzi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad