JESHI la Iran hatimaye limekiri kudungua kimakosa ndege ya abiria ya Ukraine siku ya Jumatano ya Januari 8, mwaka huu, televisheni ya taifa ya Iran imeripoti.
Taarifa ya jeshi la Iran imeeleza kuwa mkasa huo umetokana na “makosa ya kibinadamu” baada ndege hiyo kupita karibu na eneo nyeti linalomilikiwa na Kikosi cha Mapinduzi (Revolutionary Guards).
Maafisa waliofanya kosa hilo wataadhibiwa, taarifa hiyo imeeleza.
Awali Iran ilikanusha vikali kuwa moja ya makombora yake yaliitungua ndege hiyo karibu na mji mkuu wa Tehran.
Watu wote 176 ndani ya ndege hiyo wamepoteza maisha.