Iran yamuweka kizuizini balozi wa Uingereza mjini Tehran



Balozi wa Uingereza mjini Tehran, Rob Macaire, atiwa nguvuni akishiriki shughuli iliyoandaliwa kuwakumbuka wahanga  wa ndege ya abiria ya Ukraine iliyoanguka mji mkuu wa Iran, Tehran.

Katika shughuli hiyo ambayo ilifanyika mbele ya chuo kikuu cha Emir kabir, kauli mbalimbali za kuipinga serikali zilikuwa zikatolewa na inasemekana kwamba Balozi Macaire alijaribu kuandaa vitendo vya uchochezi.

Pamoja na hayo balozi huyo aliachwa huru baada ya masaa kadhaa.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Dominic Raab alisema, “ Kuwekwa kizuizuni kwa balozi wetu mjini Tehran bila hatia wala maelezo ni uvunjifu wa sheria za kimataifa”.

Marekani nayo imeonyesha kupinga tukio hilo…

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani, Morgan Ortagus, alisema  " Tunatoa wito kwa Ä°ran, iombe radhi rasmi kwa Uingereza kutokana na uvunjifu wa haki na pia iheshimu haki za wanadiplomasia wote”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad