Taarifa ya maandishi iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Iran inasema, kufuatia Macaire kufanya “vitendo visivyo vya kawaida na kushiriki katika maandamano haramu” aliitwa na wizara lakini sanjari na hilo utawala wa Tehran umetuma barua rasmi ya kupinga kitendo hicho kwa balozi huyo na kwa serikali ya Uingereza.
Kufuatia Macaire kushiriki katika maandamano ya kuipinga serikali siku ya Jumamosi mjini Tehran, Ä°ran ilimtia kizuizini kwa muda na baadaye ikamuachia huru.