Jerry Muro amuagiza OCD kuwasaka wezi wa vifaa vya NIDA Muungwana Blog · Muungwana



Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amemuagiza OCD ahakikishe Watu wasiojulikana ambao wamehusika na wizi wa vifaa vya NIDA katika kituo kidogo cha Halmashauri ya Wilaya Arusha wanajulikana na wanachukuliwa hatua za kisheria bila kumuonea Mtu.

Walinzi wa Ofisi hiyo wamesema hadi leo asubuhi wamezunguka kufanya ukaguzi nje ya jengo hilo na hawakuona dalili za tukio la wizi wala mlango kuvunjwa.

"Usinunue Laptop au camera ambayo huijui, tukikukamata na vifaa hivyo wewe ni sawa umekutwa na ngozi ya twiga au nyara nyingine ya Taifa, na kama unavyo vifaa rudisha tukivapata vifaa hivyo kwa nguvu zetu hakuna rangi utaacha ona" - Jerry Muro, DC Arumeru

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad