JOHN Mnyika Aeleza Alivyofutiwa Mtihani Kidato cha Nne

 
Mbunge wa Kibamba na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, amesema kuwa kitendo cha yeye pamoja wenzake kufutiwa mtihani wa Kidato cha Nne na hatimaye kuurudia, ndiyo kilimfanya kuachana na ndoto ya kuwa Padre na kutaka awe kiongozi.


Akizungumza leo Januari 29, 2020 jijini Dodoma, katika kipindi cha KONANI kinachorushwa na ITV, amesema kuwa mwaka 1998 yeye ni miongoni mwa wanafunzi ambao walifutiwa mitihani baada ya Mtihani wa Taifa, kuvuja karibia nchi nzima, na kuurudia tena kwa kuufanya upya mwaka 1999.

"Nimeanza siasa nikiwa Sekondari, mwaka 1998 sisi ndio wale wanafunzi ambao mtihani wetu karibu nchi nzima ulivuja na ukafutwa nchi nzima, wakati nasoma Maua Seminary, ndoto yangu ilikuwa ni kuwa Padre na kuwa Mwanasayansi, 1999 tukarudi kufanya mtihani kwa mara ya pili na hicho kitendo kilinifanya nifikirie mara mbili mbili ni uongozi gani unashindwa kusimamia mitihani isivuje?, nikafaulu kwa kupata A kwenye masomo Tisa" amesema Mnyika

Mnyika amedai kuwa kitendo cha wao kufutiwa mtihani, ndicho kilimsukuma zaidi kuingia kwenye siasa hali iliyopelekea kuona wito wake wa kuwa padre ama mtawa ni mdogo zaidi, hivyo wito wake mkuu ni kuwa kiongozi wa kufanya mabadiliko
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad