Jonesia Rukyaa Kuchezesha Simba, Yanga Jumamosi Taifa



Mwamuzi wa kati, Jonesia Rukyaa ameteuliwa kuchezesha pambano la watani wa jadi, Januari 4, 2020 kati ya Simba dhidi ya Yanga, Uwanja wa Taifa.

 

Katika mchezo huo mwamuzi Jonesia kutoka Kagera atasaidiwa na msaidizi namba moja, Sudi Lila huku namba mbili akiwa, Hamisi Chang’walu wote wa jijini Dar es Salaam.

 

Kwa mujibu wa TFF, mwamuzi wa akiba ni Elly Sasii wa Dar es Salaam huku Kamishna wa mchezo huo akiwa Khalid Bitebo w kutoka Mwanza na Mtathimini waamuzi ni Sudi Abdi ambaye anatokea Arusha.

Mwamuzi Jonesia anaingia kuchezesha mchezo wake wanne wa mechi ya watani huku akiwa na rekodi kutoa kadi nyekundu kwa michezo miwili aliyochezesha awali.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad