Kamanda Mwandamizi wa Jeshi la Iran Asema Mashambulizi Ndio Yanaanza



Kamanda mwandamizi wa jeshi la Iran amesema mashambulizi ya makombora dhidi ya maeneo ya Marekani nchini Iraq hayakulenga kuwauwa wanajeshi wa Marekani lakini yalitaka kuharibu vifaa vya kijeshi vya Marekani na ni mwanzo wa mfululizo wa mashambulizi katika eneo hilo.

Amirali Hajizadeh, mkuu wa jeshi la anga la Iran, pia amesema ulipizaji kisasi sahihi kwa Marekani kumuua jenerali maarufu wa Iran Qassem Soleimani ilikuwa ni kuyaondoa majeshi ya Marekani kutoka Mashariki ya Kati.

Pia amesema Iran ina mamia ya makombora yaliyo tayari na wakati Tehran ilifyatua makombora jana ilitumia mashambulizi ya mtandaoni kuzizuwia ndege za Marekani kuruka pamoja na mfumo wa kuendesha ndege zisizo na rubani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad