Kamanda wa Jeshi la Iran Qasem Soleimani Kuzikwa Leo



Idadi kubwa ya waombolezaji waliyovalia mavazi meusi wamejitokeza kutoa heshima za mwisho kwa kamanda wa jeshi la Iran Qasem Soleimani kabla ya kumzika.

Soleimani aliuwawa katika mapambano ya anga na jeshi la Marekani nchini Iraq siku ya ijumaa, baada ya rais Donald Trump kutoa amri kuwa auwawe.

Mwili wake sasa upo katika mji aliokuwa akiishi wa Kerman uiopo kusini mashariki mwa Iran, eneo ambalo anatarajiwa kuzikwa leo hii.

Kundi kubwa la watu tayari wamejitokeza katika shughuli hizo za mazishi mjini Tehran.

Iran iliapa kulipiza kisasi mauaji hayo ya kiongozi wa jeshi Soleimani na siku ya jumapili, ilijitoa katika vizuizi vya matumizi ya nyuklia ya 2015.

Kiongozi wa Iran, Ayatollah Khamenei akiongoza ibada ya mazishi ya Qasem Soleimani
Soleimani, alifariki akiwa na umri wa miaka 62, akiongoza kundi la jeshi la Quds ,na kazi yake kubwa ni kulinda usalama wa Iran na kuongeza ushawishi wa taifa hilo la Mashariki ya kati.

Katika mji wake, Soleimani alitambuliwa kama shujaa wa taifa na alifahamika kama mtu wa pili ambaye ana nguvu zaidi katika taifa hilo akimfuatia kiongozi wa Iran Khamenei.

Lakini sio raia wote wa Iran walimuona kuwa ni mtu mzuri.

Alikuwa kiongozi aliyeongoza jeshi kuua waandamanaji wengi mwishoni mwa mwaka 2019.

Alitumia fedha nyingi kujenga uhusiano na majeshi mengine ya Lebanon, Yemen, Iraq na Syria wakati ambao Marekani ilikuwa inaweka vikwazo vingi dhidi ya Wairan, Mhariri wa BBC Mashariki ya kati amebainisha.

Soleimani alikuwa anaungwa mkono na rais wa Syria, bwana Bashar al-Assad katika nchi ambayo ilikuwa na migogoro ya wenyewe kwa wnyewe, huku kukiwa na makundi ya kiislamu ya the Shia, Hezbollah huko Lebanon, na kuongoza kundi la kijeshi la Iraqi dhidi ya kundi la kigaidi ya kiislamu la Islamic State.

Marekani walimona kuwa gaidi na rais Trump alisema kuwa alikuwa akifanya njama za "kushambulia" wanadiplomasia wa Marekani na Majeshi ya Marekani.

Televisheni ya taifa imeonyesha mkusanyiko mkubwa wa waombolezaji katika mji wa Tehran siku ya jumatatu.Taarifa zilisema kuwa mamilioni ya watu walijitokeza , idadi ya watu hao bado haijafahamika .

Waombolezaji walipita katika jeneza la Soleimani huku wakiinamisha vichwa chini na kuimba 'kifo kwa Marekani' .
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad