Kauli ya Lipumba baada ya Madiwani CUF kuhamia CCM


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, amesema anashangazwa na kitendo cha Madiwani 8 wa Halmashauri ya jiji la Tanga waliojiengua chama hicho na kusema viongozi hao wamekwenda kuunga hali ngumu ya maisha.


Profesa Lipumba ameyasema hayo katika kikao cha ndani cha wanachama kilichofanyika jijini Tanga.

Lipumba amesema kuwa "kila mmoja analalamika kwamba vyuma vimekaza wao wanakwenda kuunga mkono vyuma vimekaza, hii ni ajabu sana"

Mwenyekiti huyo aliwapongeza Madiwani waliokataa kuyumbishwa na kusisitiza kwamba msimamo huo ndiyo utakaowasababisha wananchi kuwachagua tena katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020.

Hivi karibuni akiwa mkoani Tanga Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally aliwapokea Madiwani 8 akiwemo Naibu Meya wa jiji la Tanga.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad