Kesi ya Tito Magoti na Mwenzie Yapigwa Kalenda tena
0
January 07, 2020
Upande wa Jamhuri umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi inayimkabili Ofisa Elimu kwa Umma wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti (26) na mwenzake, Theodory Gyan (36), kuwa upelelezi katika shauri hilo upo katika hatua nzuri kukamilika.
Hayo ameyaeleza wakili wa serikali, Renatus Mkude, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la utakatishaji fedha wa zaidi ya Sh. Milioni 10 ambapo ameomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Upande wa utetezi akiwemo Wakili Anna Henga ambaye ni Mkurugenzi wa LHRC, umeomba upande wa jamhuri kuharakisha upelelezi huo ili shauri hilo liweze kusikilizwa kwa wakati.
Akijibu hoja hiyo, wakili wa serikali amesema watajitahidi kuharakisha upelelezi huo kwani mbali na kuhusisha jeshi la polisi pia unahusisha vyombo vingine.
Miongoni mwa mashitaka yao wanadaiwa Februari mosi, 2019 na Desemba 17, 2019 ndani ya jiji na mkoa wa Dar es Salaam kwa pamoja washtakiwa mengine ambao hawapo mahakamani walimiliki programu ya kompyuta iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya kutenda makosa ya jinai.
Washtakiwa hao wanasota korokoroni kwa sababu kesi yao ya uhujumu uchumi na haina dhamana
Tags