Kigwangala "Tofauti zetu na Katibu Wangu Hazikuwahi Kuathiri kazi:
0
January 10, 2020
Baada ya kumaliza tofauti zao ndani ya muda uliotolewa na Rais Magufuli, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amekutana na Prof. Adolf Mkenda, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mwanza na kusema tofauti zao hazikuwahi kuathiri kazi.
Viongozi hao pamoja na mengine wamekutana kwa ajili ya kikao cha tatu cha maandalizi ya Maonesho ya Utalii kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa, Kigoma na Tabora pamoja na Jukwaa la uwekezaji katika Sekta ya Utalii kwa Kanda Ziwa.
"Kazi zinaendelea, haya mafanikio yote yasingejitokeza kama tusingekuwa tunashirikiana, mahusiano yetu hayakuathiri hata siku moja utekelezaji wa kazi, hayo mengine madogomadogo ya kibinadamu yalishamalizwa"- Kigwangalla
Tags