Kiongozi wa kidini wa Iran ayatetea majeshi kwa kudungua ndege ya Ukraine


Kiongozi mkuu dini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ametetea majeshi ya nchi yake baada ya kukiri kuwa ilidungua ndege ya abiria ya Ukraine kimakosa.

Amesema kikosi maalum cha majeshi ya ulinzi ya Iran Revolutionary Guard - kilichohusika na mkasa huo - "kilikuwa kunalinda usalama" wa Iran.

Maandamano ya ndani ya nchi na ukosoaji kutoka mataifa ya kigeni yameiweka Iran mashakani kuhusisna na jinsi inavyoshughulikia tukio hilo.

Lakini Ayatollah alitoa tamko hilo wakati wa alipoongoza sala ya Ijumaa mjini Tehran kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012.

Ametoa wito wa "umoja wa kitaifa" na kusema kuwa "maadui" wa Iran - akiashiria Washington na washirika wake - wanatumia ajali hiyo ya ndege kuzima mauaji ya jenerali Qasem Soleimani.

"Mamilioni ya raia wa Iran na maelfu ya raia wa Iraq walimuomboleza [Soleimani]," alisema.

Ndege aina ya Boeing 737-800 ya shirika la kimataifa la ndege la Ukraine ilikuwa inasafiri kuelekea Kyiv kutoka Tehran Januari 8, ilipoanguka muda mfupi baada ya kuanza safari.

Abiria wote 176 waliokua ndani ya ndege hiyo wengi wao raia wa Iranian na Canadians, walifariki.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad