LIBYA: Kambi ya Mafunzo ya Kijeshi Yashambuliwa, Watu 28 Wafariki


Msemaji wa Wizara ya Afya, Amin al-Hashemi amesema Wanafunzi 28 wa Mafunzo ya Kijeshi wamefariki katika shambulio hilo lililofanywa kwa njia ya anga ambapo wakati wa shambulio Wanafunzi walikuwa kwenye gwaride

Wengi waliouawa walikuwa na miaka kati ya 18 na 22, huku Madaktari katika Hospitali ambazo Majeruhi na miili ilipelekwa wakisema inakuwa ngumu kutambua waliofariki kwa haraka maana wameungua vibaya au viungo vimegawanyika

Tangu Aprili 2019, Kambi za Jeshi za Serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa zimekuwa zikishambuliwa na vikosi vilivyoundwa na Kamanda Khalifa Haftar anayedaiwa kuasi na kujiunga na Wapinga Serikali Mashariki mwa Libya

Kumekuwa na ongezeko la mashambulio ya anga yanayotokea katika Mji Mkuu wa Libya, Tripoli kwa wiki za hivi karibuni, huku wasiwasi ukitanda kuwa mapigano yataongezeka zaidi baada ya Uturuki kuruhusu Majeshi yake kwenda Libya kusaidia Vikosi vya Serikali
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad