DAA---Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameviagiza Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuwashughulikiwa wale wote wanaopotosha na kudharau vyombo hivyo katika kazi yake.
“Siku hizi kumekuwa na tabia ya hovyo imejitokeza kwa baadhi ya Watanzania wachache. Kila kitu kinachofanywa ni Usalama wa Taifa, mtu akipotea siku mbili hata kama hajapotea yupo kwa mpenzi wake ni Usalama wa Taifa“ Rais Magufuli
“Niviombe vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama likiwemo Jeshi la Polisi ambao huwa mshughulikia wahalifu, msiwaache wahalifu waanze kuchafua vyombo vya Ulinzi na Usalama. Mtu akizungumza amempotea huyu ana ushahidi mshikeni mpaka atoe ushahidi“ Rais Magufuli