Mahakama ya Kisutu yafuta Kesi ya Umeya Dar



Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifuta kwa gharama kesi ya Meya wa DSM, Isaya Mwita ya kutaka kusitisha mchakato wa kumuondoa Madarakani.

Hatua hiyo inatokana na Mwita kuwasilisha maombi ya kuifuta kesi hiyo kupitia Wakili wake Hekima Mwasipu mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mtega akidai anaona kesi hiyo haina maana kuwepo Mahakamani kwa sababu hatua za kumng'oa Madarakani zilishafanyika.

”Nakubaliana na maombi ya muombaji (Mwita) ya kuliondoa shauri hili, hivyo naliondoa kwa gharama maana tumepoteza muda, rasilimali na uandaaji wa majibu kuhusu shauri hilo, hesabu zitafanyika kujua gharama zikoje na atalipia" - Hakimu Mtega

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad