Mambo ya Kuzingatia 2020 ili Kuepuka Presha Zisizo za Lazima



1. Wapeleke watoto wako shule unazomudu kulipa ada kwa sasa sio sababu mwanao anasoma shule ya gharama kubwa basi ndio atapata matokeo mazuri. Jikune unapojifikia. 

2. Panga nyumba unayomudu kulipa kodi sio kila mwaka unalazimisha kuishi kwenye nyumba za gharama kubwa wakati uwezo mdogo.

3. Mkeo ni mjamzito (au wewe mwanamke ni mjamzito) basi anza kujiandaa mapema kudunduliza pesa za 
kukusaidia unapojifungua. Una miezi tisa ya kujiandaa usianze kusumbua watu kana kwamba ni dharura. 

4. Weka Akiba zaidi na tumia kidogo. Matumizi yasizidi kipato unaingia hadi madeni ili kujionesha ufahari 2020 badilika.

5. Kula chakula bora ili kuepuka magonjwa yatokanayo na mlo hafifu. Chakula bora sio lazima kiwe ghali. 

6. Usiige kila fasheni inayoingia la msingi vaa nguo safi zilizopigwa pasi vizuri hata kama ni mitumba mradi ni safi unapendeza tu. 

7. Epuka kuazima vitu vya thamani wakati uwezo wenyewe mdogo. Unaazima gari la mtu ukiligonga huna uwezo wa kununua hata tairi hebu ridhika na ulichonacho.

8. Tumia muda mwingi kwa mambo yahusuyo roho yako. Mambo ya mwili huu ni ya muda tu wekeza muda wako kwenye mambo ya rohoni, mtafute Mungu kwa bidii, Soma neno la Mungu, kuwa mtu wa ibada itakusaidia kuepuka mashambulizi mengi ya kiroho. 

9. Usitarajie mambo mengi kwa watu. Kwa kila unachotarajia jiwekee asilimia fulani ya kukosa ili utakapokikosa usiumie moyo. Umemuomba mtu mchango jiandae kupewa au kutopewa, umemchumbia mtu jiandae kukubaliwa au kukataliwa, umemkopesha mtu pesa jiandae kulipwa au kutolipwa, kwa kila jambo jiandae kisaikolojia. 

10. Epuka madeni.
Madeni Madeni Madeni.
Yamekuwa chanzo cha huzuni kwa wengi. Epuka kukopa pesa au kuchukua vitu kwa makubaliano ya kulipa baadae. Usifanyie kazi pesa ambayo hujaishika mkononi umeahidiwa tu kuipata. Subiri uishike ndipo ununue unachohitaji.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad