Marekani yajiandaa na shambulizi la kulipiza kisasi kutoka Iran... Wanajeshi Wengine 3500 Kutumwa Mashariki ya Kati


Marekani kwa sasa inajiandaa na shambulizi la kulipiza kisasi kutoka Iran baada ya shambulizi lake la anga kumuua kamanda mkuu wa Iran, hatua ambayo imetia wasiwasi nchi zote duniani na hata kutiliwa shaka na baadhi ya wabunge wa Marekani.

Shambulizi la anga la Marekani Alhamis lilimuua Meja Jenerali Qassem Soleiman, mkuu wa kikosi cha Quds, pamoja na kamanda wa wanamgambo wa Iraq, karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad, na kuchochea vitisho vikali vya kulipiza kisasi kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.

Ikijibu tishio hilo linalozidi kuongezeka dhidi ya wafanyakazi na vituo vya Marekani katika Mashariki ya Kati, wizara ya ulinzi ya Marekani imetoa taarifa ikisema itasambaza kikosi huko Kuwait kama hatua ya tahadhari na sahihi, bila kutaja idadi ya wanajeshi.

Isikupite Hii: Ajira Mpya Zilizotangazwa Wiki Hii ...Soma Hapa

Hata hivyo vyombo vya habari vya Marekani jana vilitangaza kuwa nchi hiyo itatuma zaidi ya askari 3,500 wikiendi hii. Na askari wengine wa ziada kutoka divisheni ya 82 ya askari wa parashuti watapelekwa Iraq, Kuwait na sehemu nyingine za kanda hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad