Mchungaji Ashambuliwa kwa Kusema Apewe 10 Percent Amfufue Kobe Bryant



Mchungaji Nigel Gaisie wa nchini Ghana ameibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii huku wengi waliofikiwa na taarifa zake wakimkosoa baada ya kusema ameagizwa na Mungu amfufue Mkongwe wa Basketball Kobe Bryant na Mtoto wake waliofariki kwenye ajali ya Helikopta jumapili iliyopita.

Mchungaji huyo amesema alichokisema hajakitunga wala kukiwaza yeye bali ameoneshwa na kuagizwa na Mungu kwa njia ya ulimwengi wa kiroho na kwamba atafanya kumfufua KobeBryant na Binti yake Gianna iwapo tu atapewa asilimia 10 ya utajiri wa Kobe.


“Mungu amenionesha kupitia ulimwengu wa kiroho, nimeona Mwanaume akidondoka na Dunia yote ikitikisika, nimeona Watu wakiomboleza mitandaoni lakini bila kupewa 10% ya utajiri wake siwezi kuwafufua maana hayo ni maagizo ya Mungu”

“Mungu ameniambia niongee na Familia ya Kobe, Ubalozi wa Marekani Ghana na dunia kwa ujumla, wakubali kulipa hicho kiwango cha fedha na nitafanya kama Mungu alivyoniagiza kuwarudishia uhai Kobe na mwanae” – Nigel Gaisie

Kobe Bryant na Mtoto wake Gianna ni miongoni mwa waliofariki kwenye ajali ya Helikopta jumapili iliyopita ambapo jumla ya waliofariki ni 9 kama inavyoonekana kwenye hii picha hapa chini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad