Meya wa Jiji Achomolewa na Polisi Kikaoni
0
January 17, 2020
Kikao cha Kamati ya Fedha na Uongozi Halmashauri ya Jiji la DSM kimefanyika chini ya ulinzi wa Polisi baada ya kuibuka kwa malumbano baada ya Wajumbe wanaomtambua Isaya Mwita kuwa Meya kutaka aongoze kikao hicho huku wasiomuunga mkono wakitaka Naibu wake Abdalla Mtinika aongoze.
Inaelezwa kuwa Meya Mwita alikuwa wa kwanza kuendesha kikao hicho cha Kamati ya Fedha na Uongozi Halmashauri ya Jiji la DSM, lakini Polisi walifika na kumtoa kisha Naibu Meya Mtinika akaendelea kukiendesha chini ya ulinzi wa Polisi.
Tags