Mfahamu Ndege aliyeruka Maelfu ya Kilomkita Kutoka Ulaya mpaka Afrika Mashariki, Akutwa Amekonda


Mamlaka ya wanyama pori Kenya (KWS) imesema kuwa ndege ambaye huwa mara chache sana kuonekana, amekutwa kwenye nyavu za kuvulia huko Magharibi mwa Kenya.

Finland

Ndege huyo anasemekana kuruka kilomita 6,948 au maili 4,317 akiwa anatokea Finland.

Ndege huyo alikutwa na majeraha miguuni lakini alikuwa mzima wa afya licha ya kwamba alikuwa amekonda, mamlaka imeeleza.ndege wa Finland

Ndege huyo alijulikana asili yake kutokana na ringi aliyokuwa amevalishwa mguuni kuwa na maelezo ya asili yake kuwa makumbusho ya Finland (Museum Zool, Helsinki Finland, www.ring.ac, M-68528),” KWS ilituma maelezo.ndege

Ndege huyo anayekula samaki aligunduliwa siku ya Jumatatu na idara ya wanyama pori Kenya. Na kwa sasa yuko katika uangalizi kwa siku chache kabla ajaachiwa kwenda porini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad