Miguna Miguna Azuiwa Berlin



WAKILI wa Upinzani nchini Kenya, Miguna Miguna ameshindwa kurejea nchini humo baada ya kuzuiliwa kupanda ndege na Mamlaka ya nchini Ujerumani.

 

Miguna alitahadharishwa asiondoke Uwanja wa Ndege wa Berlin kuelekea Uwanja wa Kimataifa wa JKIA nchini Kenya au nchi nyingine yoyote Barani Afrika.

 

Zuio hili linakuja muda mchache baada ya Mahakama ya Juu ya Kenya kuagiza Serikali kumruhusu wakili huyo kurejea nchini humo. Mahakama pia imeagiza Maafisa wa Haki za Binadamu kufuatilia suala hilo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad