“Muziki kwa kiasi kikubwa ni chanzo cha mtafaruku uliosababisha mimi na mke wangu tutengane kwa sababu kuna muda nakuwa studio mpaka saa 8:00 usiku, kiasi kwamba nasinzia, nikija kushtuka saa 12:00 alfajiri na nikiangalia simu nakuta missed calls zaidi ya kumi" staa huyo ameiambia Globalpublishers na kuongeza
“Pia muda mwingine ninapokuwa kwenye shoo kawaida tu siwezi kupanda na simu stejini, lakini utakuta mke anakosa imani na mimi na ugomvi unaanzia hapo,”
"Naweza kusema tu mwanamke niliyebahatika kumuoa hakuwa na ujuzi sana kwenye masuala ya muziki, ninamaanisha ishu nzima ya mzunguko wa kazi hii na mambo yote yanayohusiana na biashara ya muziki"
Pamoja na hilo pia tatizo lingine lilitokana na kufuatwafuatwa kwenye mitandao na muda mwingine meseji zinakuwa nyingi kutoka kwa watu tofautitofauti, jambo ambalo ni kawaida kwa watu maarufu, lakini kwa mwanamke niliyemuoa hakuwa akielewa kabisa juu ya hilo" Stamina ameiambia Globalpublishers kisha kusisitiza
Globalpublishers : Unaona wanawake wanakosea wapi hasa?
Stamina: Wanakosea jambo moja tu, yaani wanataka kama mmeoana, basi mwanaume sitakiwi kuongea na mtu yeyote yule zaidi yake, jambo ambalo si zuri na halifai kwa kweli.
Globalpublishers : Wewe kama msanii unachukua hatua gani kuyakwepa hayo?
Stamina: Tasnia yetu ya muziki haitaki mambo ya kubanwabanwa hivyo kwa sababu naweza kujikuta nakosa kazi nyingi sana, kitu ambacho ninatambua na sitakiwi kukifanya ni kutokubali mtu ambaye ananitaka kimapenzi tu, lakini siyo kutokuongea naye.
Globalpublishers: Sababu gani nyingine hasa iliyosababisha ndoa yenu kuvunjika?
Stamina: Kikubwa kingine ni simu, unajua simu ni siri ya mmiliki na ndiyo maana hata Fid Q aliimba ule mstari uliosema; ‘ni ruhusa kushikana ila siyo kushikiana simu’ sasa mwenzangu alikuwa hataki kulikubali hili na ndiyo sababu mtafaruku ukawa mkubwa.
Ndoa yao ilifungwa mwezi May 2018 mkoani Morogoro