Mke wa Kobe Bryant afunguka kwa mara ya kwanza baada ya kifo cha mumewe


Wakati Dunia inaendelea kuomboleza kifo cha mkongwe wa mchezo wa basketball, Kobe Bryant na mwanaye wa kike Gianna Bryant, Mke wa mchezaji huyo Vanessa Bryant amevunja ukimya kwa mara ya kwanza baada ya kueleza mazito.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Vanessa Bryant, ameandika maelezo mazito na kuonyesha hisia kali kuhusiana na kifo cha mumewe na mtoto wake.

"Mimi na wanangu tunataka kuwashukuru watu wote waliotupa sapoti na kuonyesha upendo katiki kipindi hiki kigumu, ahsanteni kwa maombi yenu japo tulikuwa tunawahitaji sana, tumeumia  kumpoteza mume wangu ambaye alikuwa baba bora kwa watoto wake wote wanne, pamoja na mwanangu wa kike" ameandika mke wa Kobe Bryant.

"Hakuna maneno ya kutosha kueleza kiasi gani ambavyo tuna maumivu kwa sasa, sisi kama familia tuna majonzi na tunasikitika kwa kuwapoteza, itakuwa ni ngumu kuendeleza maisha bila ya uwepo wao" ameongeza.

Kobe Bryant na mwanaye wa kike Gianna, na wengine saba walipata ajali ya helikopta na kupoteza uhai wao siku ya Januari 26, 2020
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad