Mkurugenzi wa shirika la Mwanangu Development Tanzania (MWADETA), Walter Miya akiwa katika picha ya pamoja na watalii Ina Aakerberg toka Sweden na Santo (Mtanzania) baada ya kufika ‘Little Meru’ na kuweka record kwa walemavu kupanda mlima huo. (Imeandaliwa na Robert Okanda)
Kwa mara ya kwanza katika historia Ina Aakerberg mlemavu wa mgongo wazi kutoka nchini Sweden ameweka record kwa kutimiza ndoto ya maisha yake alipofanikiwa kupanda mlima Meru kwa baiskeli ya matairi matatu na kufika ‘Little Meru’ mita 3820 mwishoni mwa wiki.
Binti huyo mwenye miaka 33 alipania kupanda mlima huo ili aweke historia kwa lengo la kuchangia ujenzi wa majengo ya kuhudumia wagonjwa wa migongo wazi na vichwa vikubwa hapa nchini Tanzania.
Yeye pamoja na watalii wengine takribani 21 waliliapanda mlima huo ambao ni wa pili kwa urefu nchini kwa lengo la kutunisha mfuko wa kuchangia fedha za ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa vichwa vikubwa na migongo wazi kwenye hospitali ya Haydom Mkoani Manyara.
‘Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kufanikiwa kupanda mlima na washiriki wote walifanikiwa kupanda mlima isipokuwa wawili kutoka Ujerumani wenye uelmavu wa migongo wazi walioshia kambi ya Miriakamba kutokana na chnagamoto za kiafya, alisema Mkurugenzi wa Shirika la Mwanangu Development Tanzania (MWADETA), Walter Miya.
Kwa kiasi kikubwa malengo yametimia kwa safari yetu tuliyokadiria kupata shilingi milioni 40 hata hivyo malengo yalifikiwa japokuwa bado mahitaji ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya huduma na malazi ni makubwa kwa sasa.
“Tumefanikiwa kupata takribani milioni 50 hivi lakini tutaendelea na kufanya shughuli za kutunisha mfuko ili tufikie malengo mapana ya kupata jengo la vyumba vinne vya kulaza wagonjwa na kuwapatia huduma zingine mbalibali za mahitaji yao maalum” Alifafanua Dkt. Theresa Harbaur kutoka Ujerumani anayehudumia watoto kwenye hospitali ya Haydom Mkoani Manyara.
Tukio hilo la kihistoria lilidhaminiwa na makambuni mbalimbali chini ya usimamizi wa Shirika la Mwanangu Development Tanzania (MWADETA).