Hospitali ya Mloganzila leo imejibu tuhuma zilizoenea katika mitandao ya Kijamii ambapo watu wengi walilalamikia vifo vingi vinavyotokea katika Hospitali hiyo.
Taarifa ya hospitali hiyo imesema, wagonjwa wanaotibiwa MNH-Mloganzila wameongezeka katika makundi yote ambapo wagonjwa wa nje wameongezeka kutoka 17,115 mwaka 2018 hadi kufikia 25,493 Julai – Septemba 2019.
Pia, imetaja kupungua kwa vifo vya wagonjwa wanaofika hospitali hapo kutoka asilimia 14.9 iliyokuwepo katika kipindi cha Julai – Septemba 2018 hadi asilimia 10.4 kipindi kama hicho 2019.
Aidha, takwimu za MNH-Upanga zinaonyesha katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2018 wagonjwa waliolazwa walikuwa 12,375 ambapo kulitokea vifo 1,000 (mortality rate) ambayo ni asilimia 8.1.
Vilevile, katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2019 MNH Upanga ililaza wagonjwa 17,230 na kati ya hao vifo vilikuwa 1,673 ambayo ni asilimia 9.7 (mortality rate).
Pia, imekanusha madai ya kuwepo kwa madaktari wanafunzi walio kwenye majaribio ikifafanua kuwa kuna madaktari bingwa 52 na madaktari wa kawaida 50 na madaktari tarajali 53.