Mrema Afunguka Mawaziri na Watendaji Wanavyomtesa RAIS "Wanampa Mzigo na Kazi ya Kuwafukuza Kila Siku"

Nilienda kuwalipia wafungwa 42 na risiti ninazo, lakini Magereza hawakuwatoa. Risiti zilipokewa na Mahakama Dodoma lakini wafungwa hao waliendelea kushikiliwa Magereza hadi muda wao ukaisha.

Ndipo niliona kweli Rais Magufuli ana kazi na watu hawa (Wizara na Magereza).

Watendaji wake wanaona Rais Magufuli anahangaika usiku na mchana akitaka msongamano wa wafungwa ukome. Unajiuliza, Waziri kazi yake ni nini au huyo anayeangalia magereza kazi yake ni nini?

Watu ni wababe na jeuri, hakuna anayekusikiliza. Katika mazingira kama hayo utaachaje kufukuzwa?,

Malalamiko ya Rais ni ya kweli. Wanamtesa, hawamwelewi ndio maana huwa hawachukui maamuzi magumu. Wanampa mzigo na kazi ya kufukuza mara kwa mara, ionekane kazi ya Rais ni kufukuza- Naibu Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Pili, Augustino Mrema
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad