Msimamo wa Madee Kuhusu Goli la Kagere


Nguli wa Hip Hop nchini Tanzania na shabiki kindakindaki wa klabu ya Yanga, Madee 'Seneda' amesema kuwa hayupo katika upande wa kumlaumu mwamuzi kwenye goli la Kagere alilofunga dhidi ya Namungo FC.


Madee amesema hayo alipokuwa akipiga stori na EATV/EA Radio Digital, Madee amesema kuwa ni bahati mbaya tuu sintofahamu ya magoli yanayodaiwa ya kuotea mara nyingi hutokea kwa Simba.

"Sio tatizo la hapa nyumbani tu, nafikiri limekuwa kubwa kwa sababu yamekuwa ni matukio yanayojirudiarudia sana kwenye ligi yetu hasa wanapocheza Simba", amesema Madee.

"Kwa upande mmoja nakataa kuwalaumu moja kwa moja waamuzi, kwa sababu suala la 'offside' anatakiwa kuliangalia mwamui wa pembeni. Haya ni matatizo tuu yanatokea kwa binadamu yoyote", ameongeza.

Kagere alifunga bao la tatu na la ushindi kwa Simba kwenye ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Namungo FC, Jumatano, Januari 28, goli ambalo limelalamikiwa na wadau wengi wa soka kuwa lilikuwa ni la kuotea kwa wazi.

Tazama 'interview' nzima ya Madee hapa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad