Mtandao wa SIMU wa MTN Washutumiwa Kufadhili Magaidi


Shutuma hizo zilizotolewa katika Mahakama ya nchini Marekani siku ya Ijumaa zinadai Mtandao huo mkubwa wa simu Afrika unafadhili kwa kutoa fedha kwa Makundi ya Kigaidi Nchini Afghanistan

Katika shutuma hizo ambapo Kampuni nyingine tano zimehusishwa inadaiwa kuwa MTN ilivunja sheria ya kukabiliana na ugaidi ya Marekani

MTN inadaiwa kutoa rushwa kwa Al-Qaeda na Taliban ili wasiweze kuwekeza pesa nyingi kwa ajili ya kulinda mitambo yao nchini humo ambapo fedha hizo zinadaiwa kutumika kwenye mashambulio kati ya mwaka 2009 hadi 2017

Pia, inasemekana fedha hizo zilizotolewa na mtandao huo wa mawasiliano unaoshika nafasi ya 8 kwa duniani kote, ukiwa na Watumiaji zaidi ya milioni 240, zimetumika kununua silaha hivyo kuvunja sheria ya kupambana na ugaidi

Mwaka 2015, Kampuni hiyo ililipishwa fidia ya Dola Bilioni 5 na Serikali ya Nigeria baada ya kushindwa kudhibiti laini za simu ambazo hazikusajiliwa, ambapo fidia hiyo baadaye ilipunguzwa hadi kufikia Dola Bilioni 1.7
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad