Mtatiro aagiza wazazi wasiopeleka watoto shule kukamatwa, 50 wadakwa



WAZAZI 50 wamekamatwa na Jeshi la Polisi wilayani Tunduru Mkoa wa Ruvuma, kwa kosa la kutopeleka shuleni watoto wao waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwa kwanza.

Wazazi hao wamekamatwa kufuatia agizo la Julius Mtatiro, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, la kukamatwa kwa wazazi ambao watoto wao hawajaripoti shuleni.

Mtatiro amesema operesheni hiyo ya kukamata wazazi wa wanafunzi wasioripoti shuleni, imeanza baada ya asilimia kubwa ya watoto hao kutoripoti shuleni.

“Siku 14 baada ya shule kufunguliwa, asilimia 71 ya watoto wa kidato cha kwanza walikuwa hawajaripoti shuleni. Baada ya kutoa notisi hii na kuisimamia na kukamata wazazi takribani 50, tumeweza kudahili 60.01% ya watoto ndani ya siku 7 sawa na ongezeko la asilimia 31.01,” ameeleza Mtatiro na kuongeza;

“Katika wiki ianzayo kesho Jumatatu tutaendelea na oparesheni nzito za kuhakikisha watoto wanapelekwa shuleni, siku 7 zijazo tunataka asilimia 80 ya watoto wa kidato cha kwanza wawe wamedahiliwa na wanaendelea na masomo.”

Aidha, Mtatiro amewataka wazazi wasiopelekea watoto wao kufanya hima kutekeleza agizo hilo.

“Kwa hiyo mkianza kukamatwa sitaki kuona mtu anafika ofisi ya mkuu wa wilaya kuja kuleta vifaa, hii ndio operesheni nimeianza hapa. Hilo hamna mjadala. Mjadala wake mlete mtoto shuleni. Na ninataka kuwahakikishia. Kila mzazi atapeleka shuleni mtoto wake,” amesisitiza Mtatiro.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad