Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) mkoani Dodoma inamshikilia bw. Samwel Tuppah(37) ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Multichoice Tanzania Limited ambaye ni mchunguzi wa maudhui yasiibiwe kwa kosa la kuomba milion 5 kutoka kwa mmiliki wa wa kampuni ya Feisali Cable Network ya jijini Dodoma ili asichikue hatua kwa kampuni hiyo kwa tuhuma za za kuiba maudhui ya DSTV.
Akizungumza na wanahabari Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo amesema bwana Samweli Tuppah ambaye ni mkazi wa Tegeta Mivumoni wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam alikutwa na tukio hilo ambapo Takukuru ilianza uchunguzi wa tukio hilo tokea 2017 hadi mwaka Jana 2019.
"Uchunguzi unaonesha kuwa Kati ya Mwaka 2017 hadi 2019 bwana Tuppah aliomba na kupokea jumla ya shilingi milioni 5 Kama hongo kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya Feisal Cable Network ya Jijini Dodoma ili asichukue hatua kwa kampuni hiyo kwa tuhuma za kuiba maudhui ya DSTV" amesema Kibwengo.
Pia taasisi hiyo inatarajia kumfikisha mahakamani Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa chuo kikuu cha St John Dodoma James Gebu (27) mkazi wa Dodoma kwa kosa la kujaribu kutoa rushwa ya sh 900,000 kwa Ofisa mitihani wa chuo hicho ili awaongezee ufaulu wanafunzi wenzake 6 katika (GPA) zao kinyume na kifungu cha sheria cha 15 (1) cha sheria ya kupambana na rushwa sura ya 329 marejeo ya 2018.
Kibwengo amesema Mwanafunzi huyo wa shahada ya kwanza ya uwalimu katika chuo hicho kutokana na hilo aliwataka wanafunzi wa vyuo kuzingatia masomo ya darasani na sikutegemea kutoa rushwa ili upate ufaulu mkubwa wakati uwezo wa darasani haupo.
"Nawaomba wanafunzi jijengeeni tabia ya kusoma taifa linahitaji watu waelewa wenye uwezo wa kupeleka maendeleo mbele," amesema Kibwengo.
Mbali na hilo amesema sekta ya Ardhi inaongoza kwa kukutwa na rushwa kwa kuwa na asilimia 31.4,ikifuatiwa na Serikali za mitaa ambayo ina asilimia (22.9),huku Polisi wakiwa na aailimia 14.3, Kibwengo amesema vyama vya siasa vina asilimia 11.4,wakati Mahakama wanafikisha 4.3,Elimu wao wanafikisha asilimia 4.3,huku sekta zilizosalia zinafikisha asilimia 11.4.
Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa pale wanapoona kuna viashiria vya rushwa ili wtu hao waweze kuchukuliwa hatua.
Katika hatua nyingine Takukuru imepanga kushirikiana na jeshi la Polisi kutangaza kampeni ya UTATU na kuhamasisha kampeni ya UTATU ikiwemo kuhamasisha wananchi kutumia App ya Takukuru kutoa taarifa za za vitendo vya rushwa ya ngono na jinai nyingine.