Mwanamke Ambae Natarajia Kumuoa Miezi 4 Ijayo Ananisaliti...Ushauri Wahitajika


Habari watanzania wenzangu
Nianze moja kwa moja kuna mkasa umenifika kama mwanaume ninayetarajia kufunga ndoa miezi minne ijayo lakini imetokea sintofahamu kubwa cn kwa mwenzangu kubadilika mm
Nafanya kazi dar na yy mkoani. mwenzangu katokea kubadilika kabisa ni ugomvi usioisha mpaka imefikia hatua tunashindwa kupanga vitu kuhusiana na ndoa yetu. Pia mahari kila kitu nilishatoa na mpaka ss hv pande zote mbili zinaendelea na vikao vy shughuri.

Mabadiliko haya yametokea gafla bila hata kutibuana wala kugombana ila kutokana na upelelezi hakinifu nimekuja kujuwa kaanza mahusiano na jamaa mmoja anafanya naye kazi nimefatilia kupitia system nilizonazo za cm za kila kitu nimejuwa kuwa ananisaliti na mpaka tarehe ya kunisaliti naijuwa kanisaliti tarehe 30 /1/2017 muda wa saa 4 usiku na pia tarehe 31/1/2017 tena kanisaliti muda kuanzia saa 3 usiku kalala kwa hyo jamaa
Imeniumiza sana nikifikiria kwa sasa tulipo hiki kitu kinatokea naumia naenda kazini sio mimi nimejaribu kutaka kuchukua maamuzi mazito moyo unasita najaribu kuuliza watu kupitia indirect way wanajibu inatakiwa kuwa na subira na kuwa na uvumilivu sana ila inauma sana.

Wanandugu naombeni ushauri nifanyeje kuhusiana na hili swala kwani nikiwa peke yangu nawaza sana inanibidi nijichanganye kupiga story kwa sana ili nijisahaulishe lakini jaman naomba ushauri nifanyeje
samahani kama nitakuwa nimewaudhimnisamehe.
Ni mm mwajamii mwenzenu.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kaka utakuja juta baadae hsta kama umetoa mahari samehe au kama yanafaa kurudishwa sawa kuliko kuja juta maisha yako yootebkuna wanawake wapo wenye mapenzi ya kweli lakini huyo ni msaliti.

    ReplyDelete
  2. Pole sana ndugu yangu, na hongera kwa kulijua jambo hilo nje ya ndoa. Kama ushahidi ni 100%. Usifikiri mara mbili amua kiume kumuacha kwani wapo wengi wazuri zaidi yake na pia wenye bahati na akili ya maisha. Wapo wengine wazuri kiasi ila nyota zao zinang'aa sana.

    Huyo si mke wako na unabahati kujua hilo mapema. Atakuathiri kisaikolojia na kukuvurugia maisha kwani hutosahau milele. Hakuna mwanamke bora anayeweza kufanya hivyo ukiwa umeshalipa mahari na ndugu pande zote tayari wanamahusiano. Huyo mwanamke ni wa hovyo na Uchwara achana nae mara moja wala usihangaike kumwita na kukaa nae dharau zake na migogoro ni dalili tosha za kuwa na mtu mwingine. Ingia google uliza signs of cheating wife au girl friend utapata kila kitu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad