Mwanamke atishia kujilipua wakati ndege ikiwa angani




Shirika la habari la Urusi la Tass limesema polisi imethibitisha kuwa mwanamke aliyeilazimisha ndege kutua ghafla leo katika uwanja wa ndege wa Domodedovo hakuwa na vifaa vya mlipuko baada ya kutishia kujilipua.

Uongozi wa ndege ya Urusi ya S7 umesema mwanamke huyo alisimama katika njia baina ya viti vya ndege na kusema kuwa alikuwa na kifaa cha mlipuko.

Polisi walimzuia mwanamke huyo mara tu ndege hiyo ilipotua. Ndege hiyo ilikuwa inasafiri kuelekea Moscow kutoka Simferopol huko Crimea, eneo ambalo lilivamiwa na kuchukuliwa na Urusi kutoka kwa Ukraine mwaka 2014.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad