Mwanamke Mjamzito Atolewa Kopo la Mafuta Sehemu za Siri


Veronica Paschal (29) mkazi wa Kishili jijini Mwanza ametolewa kopo la mafuta ya kujipaka mwilini katika sehemu za siri, ikiwa ni muda mfupi baada ya kuwaeleza ndugu zake kuwa anataka kujifungua kopo.

Licha ya kutolewa kopo hilo, daktari aliyekuwa zamu katika kituo cha afya Igoma jijini hapa, Zaitun Lionge amelieleza Mwananchi leo Januari 18, 2018 kuwa mimba ya miezi sita ya mwanamke huyo ipo salama.

Tukio hilo la aina yake limetokea jana Januari 17, 2018 baada ya Veronica kufikishwa katika kituo hicho cha afya na ndugu zake waliomtoa kwenye zahanati binafsi.

“Mwanzoni hawakuonyesha ushirikiano ndio tukawambia tutafanyaje. Wakasema kuna kopo kwamba ndugu yao anataka kujifungua kopo, tukauliza kopo linazaliwaje? Amehoji na kuongeza,

“Tukawambia hilo kopo halijaingia lenyewe mtakuwa mmeliweka wenyewe. Kopo lilikuwa halionekani lakini anavyojaribu kusukuma likatokezea.”

Amesema walipomchunguza kwenye vipimo ndipo walipolibaini kopo hilo la mafuta ya kujipaka mwilini, kwamba baada ya kulitoa waliita Polisi kuchukua maelezo ya mhusika na ndugu zake.

Amesema ujauzito wa mwanamke huyo uko salama kutokana na njia kutofunguka baada ya kuondolewa kopo hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad