Mwili wa Mama mzazi mwandishi wa habari Erick Kabendera umewasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba, unatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatatu eneo la Katoma Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera.
Siku ya Jumapili mwili wa marehemu Verdiana utatolewa hospitalini na kupelekwa Rwamishenyi kwenye nyumba yake aliyokua anaishi wakati wa uhai wake na itafanyika Ibada fupi na mwili huo utalala katika nyumba hiyo hadi siku ya Jumatatu.
Baada ya hapo mwili huo utatolewa na kupelekwa katika kijiji cha Kashenge, Kata ya Katoma aneo ambalo ndipo mume wake alikuwa anaishi kipindi cha uhai wake, na ndipo alizikwa na yeye atahifadhiwa katika nyumba yake ya milele kwenye eneo hilo.
Mazishi yatafanyika bila uwepo wa Erick Kabendera hii ni baada ya Hakimu Janeth Mtega wa Mahakama ya Kisutu kusema Mahakama hiyo haina Mamlaka ya kumruhusu Kabendera kuhudhuria mazishi ya Mama yake, hivyo kuamudu arudishwe Mahabusu hadi tarehe nyingine ya kesi inayomkabili ya utakatishaji fedha January 13, 2020 na hakuna fursa ya kukata rufaa katika maamuzi hayo.