Nafasi ya Dismas Ten Yanga yachukuliwa na mchezaji wa zamani, Abeid Mziba



Klabu ya Yanga imethibitisha uteuzi wa mchezaji wa zamani, Abeid Mziba kuwa Kaimu Meneja wa timu hiyo ambaye anachukua nafasi ya Dismas Ten.


Uteuzi huo umefanyika kufuatia Dismas Ten kusimamishwa kazi na uongozi wa klabu kutokana na kitendo cha kuwavalisha sare zisizo rasmi wachezaji na benchi la ufundi, sare ambazo hazijatengenezwa na mdhamini wa vifaa vya michezo wa klabu hiyo.

Abeid Mziba maarufu kama ‘Tekero’ ni mmoja wa wachezaji mahiri wa klabu ya Yanga katika miaka ya 1980’s ambapo alishinda ubingwa wa ligi daraja la kwanza (sasa Ligi Kuu Tanzania Bara) na klabu hiyo mwaka 1987.

Alizaliwa Februari 12, 1962 Kigoma Ujiji, aliwahi kuzichezea klabu za Ufundi ya Kigoma, Reli ya Morogoro, Reli ya Dodoma kabla ya kutua Yanga ambako alicheza kwa mafanikio kuanzia mwaka 1980 hadi 1992.

Alipata umaarufu akiwa na klabu ya Yanga, hasa kwa umaliziaji wa mipira ya kichwa, kulikopelekea kupewa jina la ‘Tekero’ ambaye ni mganga wa jadi maarufu katika kipindi hicho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad