Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Stella Manyanya Atoa Rai Kwa Watafiti Kote Nchini Kufanya Tafiti Zenye Uhalisia.
0
January 16, 2020
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Serikali imesema kuwa itaendelea kuongeza jitihada kubwa ya kuhakikisha kwamba tafiti zote ambazo zina msingi na zimefanyika na wataalamu wa aina mbalimbali ikiwemo vyuo vikuu zinatumiwa kikamilifu.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Mhandisi Stella Manyanya wakati akizingumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuzindua Programu ya Miezi 18 ya kuziwezesha bidhaa zinazozalishwa nchini kuingia katika soko la kiushandani kimataifa.
Pia ametoa rai kwa watafiti kuhakikisha kuwa wanatoa utafiti wenye uhalisia kwani utafiti ni kitu ambacho kinatoa kitu ambacho kinatoa ushahidi kwa kile ambacho wanataka kukifanya na kuwataka wafaiti hao kufanya utafiti wa kweli ambao utaleta matokeo sahihi.
Mhandisi Manyanya, Ameipongeza Taasisi ya Utafiti Sera na Uchumi (REPOA) na kuwashukuru wadau mbalimbali wakiwemo nchi za ulaya kwa kuweza kuisaidia programu hiyo kwani kwa muda mrefu serikali imekuwa ikishirikiana na watafiti wa aina mbalimbali kupitia taasisi za serikali kama vyuo vikuu,NGO,s ikiwemo REPOA .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utafiti sera na uchumi (REPOA) Dkt Donald Mmari amesema programu hiyo inalenga kuangalia ni jinsi gani wanaweza kuongeza ushindani wa bidhaa zinazouzwa katika masoko ya nje pamoja na ya ndani.
Rais wa chama cha Mawakala wa forodha Tanzania (TAFA) Edward John Urio amesema kuwa Tanzania ni nchi ambayo iko vizuri kwenye upande wa kilimo huku akibainisha mapungu yaliyopo kuwa ni kwenye obora wa uzalishaji hivyo kupitia utafiti huo vyuo vyenye utalaamu kutoka uhalanzi vitaweza kuwasaidia wakulima wadogo wadogo na wale wakubwa kuweza kutoa bidhaa zenye ubora.
Lengo la Programu hiyo ni kuendela kuimarisha mahusiano kati ya watafiti mbalimbali pamoja na wataalamu ,serikali na wadau wengine ikiwemo wafanyabishara ili kuweza kuona kwamba zile tafiti ambazo zimefanyiwa kazi na kuwa na matokeo maalumu hata sera zinapotungwa kwa namna ya kushughulikia biashara waweze kutumia matokeo halisi yaliyopatikana kupitia tafiti na kuweza kufanya maamuzi yaliyo sahihi zaidi.
Tags