NECTA Yafuta Matokeo ya Watahiniwa 333


Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), limefuta matokeo yote ya watahiniwa 333, waliofanya udanganyifu katika mitihani yao, ukiwemo mtihani wa upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne(SFNA), mtihani wa kidato cha Pili (FTNA) na kidato cha Nne (CSEE).

Akitangaza matokeo hayo leo Januari 9, 2020, Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde, amesema kuwa watahiniwa walifutiwa matokeo ni waliofanya udanganyifu.

“Kati ya watahiniwa waliobainika kufanya udanganifu, watahiniwa 142 ni wa Darasa la Nne, 29 ni wa kidato cha Pili na 162 ni wa kidato cha Nne, ambapo pia tumezuia matokeo ya watahiniwa 538, ambao walipata matatizo ya afya na wote walipata fursa ya kufanya tena mitihani kwa masomo ambayo hawakufanya” amesema Dkt Msonde

Aidha katika matokeo hayo jumla ya watahiniwa 340,914 wa kidato cha Nne waliofanya mitihani yao kwa mwaka 2019 sawa na asilimia 80.65, kati ya watahiniwa 422,722, wamefaulu.

Katika matokeo hayo, Dk Msonde ametangaza wanafunzi 10 bora kitaifa ambapo kati yao sita wanatoka shule ya Sekondari Francis Girls ya Jijini Mbeya na aliyeongoza ni msichana Joan Ritte.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad