NEMC yanasa mifuko feki Njombe
0
January 23, 2020
Takribani mifuko 1500 ambayo thamani yake haijafahamika imekamatwa halmashauri ya mji wa Njombe na Mamlaka ya Taifa ya Uhifadhi wa Mazingira (Nemc) Nyanda za Juu Kusini katika zoezi la oparesheni la kushitukiza lililofanywa na maafisa wa Nemc.
Afisa Mazingira Nemc Nyanda za Juu Kusini, Milton Mponda amesema zoezi la utekelezaji wa sheria ya katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki iliyoanza kufanya kazi tangu Juni Mosi Mwaka 2019 limeendelea kufanywa na Maafisa wa Mamlaka ya Taifa ya Udhibiti wa Mazingira (Nemc).
TMA yatoa tahadhari upepo mkali na mawimbi Baharini
Baada ya kufanya zoezi hilo katika halmashauri ya mji wa Njombe wamewakamata wafanyabishara wakiwa wanauza mifuko ambayo haijakidhi viwango vya ubora wa shirika la viwango Tanzania (TBS) ambapo sheria ya kupigwa faini papo hapo ilitumika.
Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara waliokutwa na makosa wamejitetea kwakuadi mifuko wanayouza wanaagiza kutoka jijini Dar es Salaam ikiwemo vifungashio vya kubebea nyama kwenye bucha.
Tags