Nick Gordon, aliyekuwa mpenzi wa marehemu Bobbi Kristina Brown, amefariki akiwa na miaka 30



Joe S Habachy ambaye ni mwanasheria wa Gordon aliyekuwa mtoto wa kuasili wa marehemu Whitney Houston, hajaweka wazi sababu za kifo za kijana huyo.



Ameiambia Sky News, “kutokana na changamoto nyingi alizokutana nazo miaka ya hivi karibuni, alilazimika kutumia nguvu nyingi kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa, jambo ambalo lilishindikana.”

Gordon alikuwa yatima, marehemu  Whitney Houston alimchukua na kumlea kama mwanaye wa kuasili, baada ya kuachana na aliyekuwa mumewe Bobby Brown mwaka 2007.

Alikuwa akimwita Whitney mama, ingawa haikuwa rasmi na wala hakumuandika katika urithi wake.

Mwaka 2012, Whitney alifariki akiwa na miaka 48 katika ajali ya kuzama katika jakuzi kwenye hoteli eneo la Beverly Hills, California.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad